(Falsafa ya twahara) ndio mada iliyokua ikizungumzwa na Atabatu Abbasiyya tukufu mwezi mzima wa Ramadhani.

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya mwezi wa Ramadhani kitendo cha Dini kila siku Alasiri kilikua kinatoa muhadhara kwa aili ya kuongeza uwelewa wa Dini na imani kwa waumini, mada iliyokua inazungumzwa katika mihadhara hiyo ni (Falsafa ya twahara), ikiwa ni njia nzuri ya kunufaika na mwezi mtukufu wa Mwenyezi Mungu.

Mihadhara hiyo ilikua inatolewa kila siku Alasiri ndani ya ukumbi mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), Shekhe Ali Mujan alikua anapanda mimbari na kuelezea maana ya twahara na umuhimu wake katika ibada zote na uhai kwa ujumla, huku akifafanua vipengele mbalimbali vya kifiqhi na kiitikadi.

Mihadhara hiyo ilikua inahudhuriwa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya pamoja na mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), iliwaimarisha katika utendaji wa ibada na kuwakumbusha majukumu yao kidini na kiitikadi.

Fahamu kua kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kila mwaka hua kinaendesha mihadhara ya dini ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kila siku katika haram ya Abulfadhil Abbasi, mihadhara hiyo hujikita katika mada moja, Ramadhani ya mwaka jana ilizungumzwa mada ya swala, na Ramadhani ya mwaka huu imezungumzwa (Falsafa ya twahara) ukitaka kuangalia mihadhara hiyo ingia katika linki ifuatayo: https://alkafeel.net/videos/watch?key=11d79065
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: