Kitengo cha Dini kimetoa huduma za mafundisho kwa wingi ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa maelekezo ya kisheria katika mwezi wa Ramadhani kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kilikua kikijibu maswali kutoka kwa mazuwaru kupitia vituo tofauti ndani na nje ya ukumbi wa haram tukufu.

Rais wa kitengo cha Dini Shekh Swalahu Karbalai ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kutokana na wingi wa mazuwaru kitengo cha Dini kiliamua kufungua vituo vipya ndani ya ukumbi wa haram tukufu, na kuongeza idadi ya nashekhe kwa ajili ya kutoa ufafanuzi na kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa mazuwaru, sambamba na kufundisha mada tofauti”.

Akaongeza kua: “Hali kadhalika mashekhe walikua wanajibu maswali kutoka kwa wakina mama kwa njia ambayo sio ya moja kwa moja, na walikua wanatoa mihadha kila siku ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kila baada ya muhadhara walikua wanakusanya maswali kutoka kwa mazuwaru, na waliyajibu kwa wazi ili watu wote wafaidike kutokana na majibu hayo”.

Fahamu kua kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kilikua kimeandaa ratiba maalum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, iliyokua na kipengele cha kutoa mihadhara ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: