Hivi punde: Ofisi ya Marjaa Dini mkuu yatangaza kua kesho Jumatano ni siku ya kwanza ya sikukuu ya Idul-Fitri.

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani imetangaza kua kesho siku ya Jumatano (5 Juni 2019m) ni siku ya kwanza ya Idul-Fitri tukufu sawa na tarehe mosi Shawwal (1440h).

Hivyo tunatoa pongezi kwa waislamu na Maraajii wetu watukufu pamoja na raia wa Iraq na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kote duniani, tunamuomba Mwenyezi Mungu akubali ibada zetu, awape neema ya amani na utulivu wananchi wa Iraq na awarehemu mashahidi wa Iraq na kuwaweka mahala pema peponi na awaponye haraka majeruhi hakika yeye ni mwingi wa kusikia dua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: