Kwa picha: Mazingira ya mwezi wa Ramadhani katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f).

Maoni katika picha
Kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni sawa na vitengo vingine katika kuwahudumia mazuwaru, katika mwezi wa Ramadhani kitengo hicho kiliandaa ratiba ya kuimarisha usalama na kutoa huduma kwa namna ambayo iliwawezesha mazuwaru kufanya ibada kwa amani na utulivu.

Waliandaa kumbi za wanaume na wanawake, na kuweka mahitaji yote ya lazima, yanayo muwezesha mtu kufanya ibada kwa amani na utulivu, sambamba na kugawa vyakula vyepesi wakati wa adhana ya Maghribaini, ikiwa ni maji, tende na maziwa, pamoja na kugawa chai siku zote za mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Halikadhalika kitengo kiliandaa sehemu maalumu ya kujibu maswali kisheria ndani ya Maqaamu tukufu, waliandaliwa mashekhe maalumu waliokaa na kujibu maswali kutoka kwa mazuwaru.

Wakati huohuo Maqaam imeadhimisha matukio yoto yanayo husu watu wa nyumba ya Mtume (a.s) yaliyo tokea ndani ya mwezi wa Ramadhani, kama kuzaliwa kwa Imamu Hassan na kifo cha baba yake kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: