(Kwaheri kwaheri ewe mwezi wa Mwenyezi Mungu)… Maneno ya kuaga mwezi wa Ramadhani yasikika katika minara ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Kwaheri kwaheri ewe mwezi wa Mwenyezi Mungu.

Kwaheri kwaheri ewe mwezi wa kusimama.

Kwaheri kwaheri ewe mwezi wa twaa na maghfira.

Kwaheri kwaheri ewe mwezi wa wema na ihsaani.

Maneno hayo na mengine yamesikika kwa kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani katika mji mtukufu wa Karbala, kama ulivyo pokewa na malalo mawili matakatifu ya bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) leo hii unaagwa kwa huzuni na kumuomba Mwenyezi Mungu aurudishe tena mwakani kwa amani na usalama.

Ni desturi ya Ataba mbili tufu kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kaswida zinazo somwa na sauti nzuri inayo ashiria huzuni, ambazo husikika kupitia minara yake, na wakati huohuo huashiria furaha kwa kuingia sikukuu ya Idi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: