Kwa picha: Swala ya Idul-Fitri katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo ya pembezoni mwake.

Maoni katika picha
Katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeswaliwa swala ya Idul-Fitri, waumini wamejitokeza kwa wingi kuja kuswali swala hiyo ambayo ni hitimisho la funga zao na kilele cha ibada walizo fanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kutokana na wingi wa watu waliokuja kuswali swala hiyo, imelazimika kuswaliwa zaidi ya mara moja kwa sababu ya udogo wa eneo la kuswalia na ili kuwapa fursa ya kuswali waumine wengi zaidi bila kuathiri harakati za mazuwaru.

Waumini wamemuomba Mwenyezi Mungu mtukufu adumishe amani na utulivu katika taifa la Iraq, na awarehemu mashahidi wa Iraq na kuwaponya haraka majeruhi.

Hali kadhalika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu umefurika maelfu ya waumini waliokua wakiswali swala ya Idi.

Vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu vimefanya kazi kwa bidii na ustadi mkubwa kuhakikisha watu wote wanafanya ibada kwa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: