Kutokana na kuingia sikukuu ya Idul-Fitri Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa pongezi kwa Imamu Mahadi (a.f) na Maraajii watukufu pamoja na waislamu wote, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu airudishe tena siku hii kwa waislamu wakiwa na salama na wenye afya njema, na alitunuku taifa letu amani na utulivu, na alinde umoja wetu na kuvunja njama za maadui wetu hakika yeye ni mwingi wa kusikia, mwingi wa kujibu.