Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa ulinzi na utumishi, iliyo uandaa kwa ajili ya kuwapokea mazuwaru waliokuja kutoka ndani na nje ya nchi ya Iraq kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya mwezi wa Ramadhani, mafanikio hayo yametokana na juhudi za watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na ushirikiano wa mazuwaru watukufu, kila mmoja amefanya kazi kwa bidii kulingana na kitengo chake, watumishi wote wameongozwa na kauli mbiu isemayo (kumtumikia zaairu aliyefunga ni fahari yetu) kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu pamoja na radhi za mwenye malalo hii Abulfadhil Abbasi (a.s).
Ramadhani ya mwaka huu imekua na ongezeko kubwa la mazuwaru tofauti na ramadhani zilizo pita, na wamepewa huduma muwafaka kulingana na wingi wao, vitengo vya Ataba viliweka mazingira mazuri ya kutekeleza ibada na ziara kwa amani na utulivu.