Mwisho wake ni miski: Maahadi ya Quráni tukufu imefunga ratiba ya usomaji wa Quráni katika mwezi wa Ramadhani na kutoa zawadi kwa washiriki wake.

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya Jumanne (29 Ramadhani 1440h) sawa na (4 Juni 2019m) ndani ya ukumbi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), imefunga ratiba ya usomaji wa Quráni ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani iliyo anza tangu siku ya kwanza ya mwezi huo kwa kusomwa juzu moja kila siku, usomaji huo ulikua unasikilizwa na kufuatiliwa na mazuwaru wengi pamoja na kurushwa moja kwa moja na vituo vya luninga.

Katika hafla ya ufungaji imesomwa nusu ya pili ya juzuu la thelathini kuanzia surat Dhuha hadi mwisho, iliyo somwa na kikundi cha wasomaji wa Quráni, tahliil na takbira kisha wakasoma dua ya kuhitimisha Quráni tukufu, halafu wakapewa zawadi wale walioshiriki katika ratiba ya usomaji wa Quráni mwezi mzima wa Ramadhani.

Mkuu wa Maahadi ya Quráni tukufu Shekh Jawadi Nasrawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hafla hii hufanywa kila mwaka katika usiku wa Idi kwa ajili ya kufunga ratiba ya usomaji wa Quráni tukufu na kutoa zawadi kwa wale walioshiriki kusoma Quráni siku zote za mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wajumbe wa kamati ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni na matawi yake wamesimamia vikao vya usomaji wa Quráni ndani na nje ya mji wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: