Kiwanda za kutengeneza barafu kimetoa zaidi ya vipande elfu kumi na saba (17,000) vya barafu kwa mazuwaru na mawakibu za kutoa huduma ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, barafu hizo hubebwa na magari maalum ya kiwanda na kupelekwa katika mahodhi ya maji yaliyopo ndani na nje ya haram tukufu ya Abbasi, pamoja na kuzipa mawakibu na vikundi vya kutoa huduma sambamba na kugawa moja kwa moja kwa mazuwaru.
Idara ya maji ilibeba jukumu la kusambaza barafu katika mahodhi yaliyopo mji mkongwe wa Karbala pamoja na ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika eneo la katikati ya haram mbili kwa kutumia gari zake maalum, hali kadhalika iligawa barafu hizo kwa mawakibu na vikundi vya kutoa huduma kwa mazuwaru pamoja na kuwapa moja kwa majo baadhi ya mazuwaru.
Kazi ya kusambaza barafu ilifanywa kila siku chini ya jopo maalum lililo kua linafuatilia hali ya barafu katika mahodhi ya maji.
Fahamu kua huduma hii pamoja na zingine zilikua katika mkakati maalum uliowekwa na Atabatu Abbasiyya wa kuwahudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi, sambamba na kuwahudumia wakazi wa maeneo yanayo zunguka haram tukufu ya Abbasi.