Zaidi ya zulia (700) zilitandikwa katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili kwa ajili ya swala ya Idul-Fitri

Maoni katika picha
Idara ya kutandika miswala (zulia) katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, imefanya kazi kubwa ya kuandaa uwanja huo kwa ajili ya swala ya Idul-Fitri, imetandika zaidi ya zulia (700) kwenye eneo hilo kwa ajili ya kuwezesha kuswali waumini wengi zaidi.

Kiongozi wa idara ya kutandika miswala ustadh Muhammad Swalehe Mahadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Siku tatu za mwisho katika mwezi wa Ramadhani tumetoa stoo zaidi ya zulia (700) na kuja kuzitandika katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kazi hiho ilifanywa kwa nyakati mbili tofauti, kabla ya muda wa kufuturu na baada ya futari, tulafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na watumishi wa vitengo vingine vya eneo la katikati ya haram mbili tukufu”.

Akaongeza kua: Usiku wa kuamkia siku ya Idi tulitandika zaidi ya zulia (700) nyekundu zenye nakshi nzuri zinazo endana na utukufu wa eneo hilo, tukatandika pia katika eneo lililo pauliwa ambalo liliandaliwa rasmi kwa ajili ya kuswalia wanawake.

Akafafanua kua: “Tuliacha wazi sehemu za kupita mazuwaru wanao toka na kwenda katika moja ya Ataba mbili tukufu kwa kukatisha katika uwanja huo, wakati wa kuswali sehemu zote zilifungwa kwani uwanja mzima ulijaa watu wanaoswali, maelfu ya waumini walikuja kuswali katika eneo hilo lililopo karibu na malalo ya bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akasema: “Baada ya kumaliza swala tulianza kazi mara moja ya kusafisha mazulia kwa kusaidiwa na ndugu zetu watumishi wa idara zingine, kisha tukarudisha kwenye stoo ziliko toka”.

Akasisitiza kua: “Kazi ya kurudisha zulia hizo ilifanywa na magari yaliyo chini ya kitengo chetu, watumishi wetu wamefanya kazi kubwa katika kufanikisha zowezi hilo kwa kushirikiana na vitengo tofauti vya eneo la katikati ya haram mbili tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: