Kuna uhusiano wa kiroha kati ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na malalo takatifu, ambao huongezeka kila wakati, jana umeondoka mwezi mtukufu wa Ramadhani ulio shuhudia ongezeko kubwa la waumini waliokuja kufanya ibada jirani na malalo ya Karbala, na leo siku ya pili ya sikukuu ya Idul-Fitri wamefurika tena kufanya ibada za usiku wa Ijumaa.
Wamejaa katika haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kwenye uwanja wa katikati ya haram hizo tukufu, atabatu Abbasiyya imeweka kila kitu kinacho hitajika kwa ajili ya kufanya ibada kwa amani na utulivu.
Atabatu Abbasiyya ilitangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa ulinzi wa amani na utowaji wa huduma, katika kuwapokea mazuwaru waliokuja kutoka ndani na nje ya Iraq kumzuru Imamu Husseuin na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya mwezi wa Ramadhani, mafanikio hayo yalitokana na juhudi za watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na ushirikiano wa mazuwaru watukufu, watumishi wote walifanya kazi kwa kujituma chini ya kauli mbiu isemayo (Kumtumikia zaairu aliyefunga ni fahari kwetu), wakitafuta radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu pamoja na radhi za mwenye malalo hii Abulfadhil Abbasi (a.s).