Mradi wa kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu ni moja ya miradi inayo simamiwa na idara ya Tahfiidh ambayo ipo chini ya Maahadi ya Qur’ani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, mradi unakusudia kuandaa mahafidhi wa umri tofauti, matunda ya mradi huu yameanza kuonekana.
Tumeongea na Shekh Jawadi Nasrawi mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu amesema kua: “Hakika Maahadi chini ya ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu itaendelea kusimama pamoja na wanafunzi wake wanaohifadhi Qur’ani hadi wamalize kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, Maahadi na watumishi wake watafanya kila wawezalo kuhakikisha lengo linatimia”.
Ameyasema hayo alipo hudhuria mashindano ya kuhifadhi Qur’ani yanayo simamiwa na idara ya Tahfiidh chini ya Maahadi, Nasrawi akasisitiza kua: “Idara ya Tahfiidh inatilia umuhimu ushiriki wa wanafunzi wake katika ratiba za kimalezi na kiimani”, akawahusia vijana wanao hifadhi Qur’ani wahakikishe wanayafanyia kazi kwa vitendo yale wanayo soma ndani ya Qur’ani tukufu.
Akawashukuru wasimamiaji wa ratiba hii na walimu wa Qur’ani kwa juhudi kubwa wanayofanya, akawataka waendelee hivyo kwani jambo hili ni tukufu sana duniani na akhera.
Kumbuka kua mashindano ya kuhifadhi Qur’ani yanayo simamiwa na idara ya Tahfiidh chini ya Maahadi yanafanyika katika mji wa Imamu Hassan (a.s), yanahusisha wanafunzi wa Maahadi peke yao, wanashindano wao kwa wao, wapo makundi saba ambayo ni: (walio hifadhi juzu moja, juzu tatu, juzu tano, juzu kumi, juzu kumi na tano, juzu ishirini na walio hifadhi Qur’ani nzima).