Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ametembelea mazaru ya Aun bun Abdullahi (r.a).

Maoni katika picha
Miongoni mwa ziara zinazo fanywa na ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, makamo katibu mkuu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi akiongozana na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi bwana Jawadu Hassanawi wametembelea mazaru ya Aun bun Abdillahi (r.a) katika mkoa mtukufu wa Karbala.

Wakapokewa na katibu maalumu wa mazaru hiyo Ustadh Abdullahi Amrani Maamuri, baada ya kufanya ziara na kusoma dua akawaonyesha mikakati na hatua za ujenzi wa mazaru hiyo, pamoja na kufafanua kiwango cha ujenzi kilicho kamilika katika mradi mkubwa zaidi wa ujenzi unaotekelezwa na uongozi mkuu wa mazaru tukufu kwa kusaidiana na serikali ya eneo hilo pamoja na wahisani.

Mwishoni mwa ziara hiyo makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya akapongeza maendeleo mazuri ya mazaru hiyo, na akasema kua Atabatu Abbasiyya ipo tayari kutoa msaada wa kiufundi na kihandisi pamoja na kufungua milango ya ushirikiano, wakaagana kwa furaha kama walivyo pokelewa.

Kumbuka kua mazaru hiyo ipo umbali wa kilometa (10) kutoka katikati ya mji wa Karbala, na hutembelewa na mazuwaru wakati wote, mji huo ni sawa na eneo la kupumzika mazuwaru pia ni lango pekee la kuingilia Karbala upande wa kaskazini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: