Atabatu Abbasiyya inanafasi muhimu katika kipindi hicho, imefanya juhudi ya kutoa huduma bora kadri iwezekanavyo kwa mazuwaru watukufu na raia wa Iraq na duniani kwa ujumla katika mambo mbalimbali.
Katika taarifa hii tunataja baadhi ya miradi iliyo fanywa na Atabatu Abbasiyya katika miaka hiyo, Naya ni:
- - Kusanifu na kutengeneza dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Kutengeneza na kutia dhahabu minara miwili ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Mradi wa upanuzi wa Atabatu Abbasiyya hadi kufikia mita za mraba elfu thelathini (30,000).
- - Kupanua haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuezeka uwanja wa haram hiyo tukufu.
- - Kusanifu na kujenga hospitali ya rufaa Alkafeel katika mkoa wa Karbala.
- - Kusanifu na kujenga hospitali ya Alkafeel katika mkoa wa Baabil (ujenzi unaendelea).
- - Ujenzi wa korido za ghorofa ya pili katika Atabatu Abbasiyya.
- - Ujenzi wa nyumba za makazi za Abbasi (a.s) zipatazo (829) pamoja na shule, vituo vya biashara, zahanati na barabara.
- - Mradi wa kituo cha kuegesha magari, gereji na huduma zingine.
- - Mradi wa kukarabati maqaam ya Imamu Mahadi (a.f).
- - Mradi wa majengo ya kutoa huduma ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika barabara ya (Najafu – Karbala).
- - Mradi wa kituo cha kibiashara Al-Afaaf.
- - Mradi wa jengo la Idhaatul-Kafeel ya wanawake na Maahadi Alkafeel ya masomo ya ufundi na kukuza vipaji.
- - Mradi wa jengo la Shekh Kuleini kwa ajili ya kutoa huduma kwa mazuwaru katika barabara ya (Bagdad – Karbala).
- - Kukarabati na kuweka dhahabu katika nguzo zilizokua zimetiwa dhahabu ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Mradi wa viyoyozi (AC) katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Jengo la wageni la Imamu Haadi (a.s).
- - Jengo la kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s) kwa ajili ya harakati za wanawake.
- - Mradi wa jengo la viwanda na godauni (Saqaa/2).
- - Mradi wa kukarabati na kuweka marumaru katika kubba tukufu.
- - Mradi wa kukarabati na kuimarisha kuta za sardabu ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Mradi wa ujenzi wa vyoo katika barabara ya (Baabil – Karbala).
- - Mradi wa ujenzi wa vyoo karibu na mlango wa Kafu.
- - Mradi wa kuziba mipasuko ya ardhi katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuweka Cementi.
- - Mradi wa kituo cha Atabatu Abbasiyya tukufu cha kusafisha maji.
- - Mradi wa kiwanda cha kutengeneza barafu.
- - Mradi wa umeme wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu.
- - Ujenzi wa sehemu za kutawadhia na maji ya kunywa katika barabara ya Abbasi (a.s).
- - Mradi wa magodauni na viwanda Saqaa/1.
- - Mradi wa makhatibu.
- - Majaribio ya kihandisi.
- - Mradi wa magodauni na viwanda Saqaa/3.
- - Kiwanda cha kufyatua tofali za bloko.
- - Mradi wa majengo ya vyoo ya kwanza.
- - Mradi wa uthibitisho wa kihandisi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Mradi wa magodauni ya miswala.
- - Kiwanda cha kutengeneza tofali za mapambo.
- - Mradi wa kuimarisha ukuta wa nje wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Mradi wa kiwanda cha Kasarah.
- - Mradi wa kutoa huduma wa Saaqi.
- - Mradi wa jengo la vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Mradi wa kituo maalum cha umeme wa nyumba za makazi za Alkafeel.
- - Mradi wa magodauni na vifaa vya mapambo.
- - Mradi wa upanuzi wa Maqaam ya Imamu Mahadi (a.s).
- - Mradi wa kusoma na kufundisha/2.
- - Mradi wa magodauni (awamu ya kwanza/ ya Alwafaa).
- - Majengo ya viwanda na magodauni katika barabara ya (Najafu – Karbala).
- - Sehemu ya pili ya mradi wa magodauni ya Ataba tukufu.
- - Mradi wa matangazo mubashara (SNG).
- - Maahadi Alkafeel kwa wenye mahitaji maalum.
- - Maahadi Alkafeel ya masomo ya ufundi na kukuza vipaji.
- - Kituo cha Alkafeel cha uchapishaji.
- - Maahadi ya Qur’ani tukufu (mahsusi kwa ajili ya harakati za Qur’ani na fani zake).
- - Kituo cha masomo ya kiislamu na kimkakati.
- - Mji wa mazuwaru katika barabara ya Hilla.
- - Mji wa mazuwaru katika barabara ya Najafu.
- - Kusanifu na kujenga kiwanda cha uchapishaji wa vitabu na usambazaji cha Darul-Kafeel.
- - Mradi wa maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Kituo cha Barakaat Abulfadhil Abbasi (a.s) cha ufugaji wa kondoo.
- - Mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Vitalu vya Atabatu Abbasiyya tukufu vya mauwa na asali (ufugaji wa nyuki).
- - Shirika la Aljuud la kilimo cha kisasa na teknolojia ya viwanda.
- - Kiwanda cha A’araaf cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Mradi wa kupanua milango ya Atabatu Abbasiyya.
- - Mradi wa kituo cha mawasiliano na kudhibiti amani na usalama.
- - Mradi wa kujenga mnara wa saa ya Atabatu Abbasiyya na kununua saa mpya.
- - Mradi wa mawasiliano ya wayaless katika jengo la chini la Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Mradi wa kufua umeme kwa ajili ya matumizi ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Mradi wa shamba la Saaqi la aina adimu za tende.