Madaktari wa mradi wa (matibabu bila malipo) katika hospitali ya rufaa Alkafeel wanaendelea kutoa huduma bure kwa kutibu zaidi ya wagonjwa (120) mayatima katika mkoa wa Bagdad.

Maoni katika picha
Kikosi cha madaktari wa mradi wa (matibabu bila malipo) kwa kushirikiana na taasisi ya Al-Birru Rahim Alkhairiyya, wametoa huduma ya matibabu bure kwa mayatima wa mashahidi wa Hashdi Sha’abi na jeshi la serikali zaidi ya (120) katika mkoa wa Bagdad.

Afisa uhusiano wa hospitali hiyo ustadh Hassan Aaridhwi amesema kua: “Shughuli hii ni miongoni mwa ratiba inayo tekelezwa na jopo la madaktari wa mradi wa (matibabu bila malipo) katika mikoa yote ya Iraq, huu ni msafara maalumu kwa baadhi ya watoto wa mashahidi wa Hashdi Sha’abi katika mkoa wa Bagdad, baada ya kufanyiwa vipimo wamepewa matibabu na wengine kupelekwa katika hospitali ya Alkafeel kwa matibabu zaidi”.

Kwa maelezo zaidi angalia video.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: