Tambua mustakbali wa chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel kinatarajia kua taasisi bora zaidi ya kielimu, kinaweza kufikia viwango vya kimataifa vya ufundishaji na kufanya tafiti za kielimu zenye matokeo chanya katika jamii, na kuleta maendeleo ya kudumu katika jamii na taifa kwa ujumla.

Kwa hiyo kinafanya kila kiwezalo kujiendeleza kielimu katika sekta zote, kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya soko la ajira la Iraq chini ya mkakati maalum, malengo ya baadae yako kama ifuatavyo:

Kwanza: kufungua vitivo na vitengo vipya vya elimu.

Pili: kuajiri walimu wenye uwezo mkubwa.

Tatu: kuboresha ufundishaji na kufikia kiwango cha kimataifa.

Nne: kuandaa tafiti za kielimu na kuzisambaza katika majarida ya elimu za juu, kwa lengo la kukuza harakati za kielimu katika vitengo vya Atabatu Abbasiyya, na kutatua changamoto za jamii.

Tano: kuratibu harakati za kitamaduni (Nadwa, warsha, makomgamano ya kielimu ya kitaifa na kimataifa), kwa lengo la kukuza uwezo na kutambua harakati na maendeleo ya elimu mbalimbali.

Sita: mkakati wa kuanzisha masomo ya juu.

Saba: kufungua milango ya ushirikiano na vyuo vikuu vya Iraq na vya kimataifa na kusaini mikataba ya ushirikiano wa kielimu na kitamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: