Kitengo cha malezi na elimu ya juu kinafanya mkutano wa kujadili mikakati ya kupokea mwaka wa masomo (2019-2020m).

Maoni katika picha
Miongoni mwa mikutano ya walimu na viongozi wa idara, kamati ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imekutana na idara za shule za Al-Ameed, na vikundi vingine vya wafanya kazi kwa ajili ya kujadili mwenendo wa elimu, wamejadili mkakati wa elimu wa mwaka mpya wa masomo sambamba na namna ya kuwapokea wanafunzi wapya, kuanzia darasa la kwanza katika shule za msingi hadi elimu za juu, vilevile wamejadili ratiba ya masomo ya msimu wa joto (kiangazi) pamoaja na kuangalia mahitaji ya watumishi.

Kuhusu swala hilo Dokta Mushtaqu Ali makamo kiongozi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu amesema kua: “Mkutano wa leo pamoja na viongozi wa idara na makundi mengine ya watumishi ni hatua ya kwanza ya kuweka mkakati wa kuandikisha wanafunzi wa mwaka ujao wa masomo, tunaweka mipango madhubuti kwa awamu ijayo, jambo la pili tumejadili mahitaji ya walimu na watumishi wengine”.

Akaongeza kua: “Maendeleo ya taasisi yeyote huletwa na watendaji wake, wao ndio nguzo muhimu ya kufaulu kwa taasisi, kwa sababu maendeleo huhitaji utendaji wa vitendo wala sio nadharia, kwa hiyo maamuzi yote muhimu yanafanywa kwa kushirikiana na idara za kiutendaji ili waweze kufanya kazi wakiwa tim moja”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: