Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) kinatoa mwaliko wa kuhudhuria uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la Alwafaa la kwanza

Maoni katika picha
Katika kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu kutolewa fatwa tukufu ya kujilinda, iliyo tolewa na Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani, kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) kinatoa mwaliko wa kuhudhuria uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la Alwafaa la kwanza litakalo julikana kama (Daru Ummul Mu-uminiin –a.s-) kwa ajili ya makazi ya familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika mji wa Karbala mtaa wa Mulhaqu Alfaaris, siku ya Alkhamisi ijayo sawa na (13/06/2019m) saa kumi na mbili jioni.

Katika siku hiyo pia utafanyika uzinduzi wa (kifaru cha Alkafeel/1) kilicho buniwa na kutengenezwa na watalam wa kiiraq katika kikosi cha 26.

Fahamu kua kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) kinaendelea kutoa misaada ya kibinaadamu katika miji mbalimbali hapa nchini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: