Kwa picha: Hatua ulipofika mradi wa kituoa cha kiislamu cha masomo ya kimkakati.

Maoni katika picha
Mradi wa jengo maalum la kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati umepiga hatua kubwa sana, kazi inayo endelea hivi sasa ni ya kumalizia kufunga umeme kwenye jengo.

Tunakuletea picha za kazi zilizo kamilika katika jengo hilo ambalo lipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu chenye makao makuu mjini Najafu nacho ni miongoni mwa vitengo muhimu.

Fahamu kua mradi huu unatekelezwa na shirika la ujenzi la Anwaar chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, linajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (890) nalo ni jengo la ghorofa saba, limewekewa vionjo vya kiufundi vinavyo endana na kituo hicho na kukidhi mahitaji ya sasa na baadae, kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya kimesha tekeleza makumi ya miradi mikubwa na mamia ya miradi midogo na ya kati (ukiwemo mradi huu) ndani na nje ya Ataba tangu kuanzishwa kwake baada ya kuanguka utawala uliopita, asilimia kubwa ya miradi imefanywa na raia wa Iraq, na miradi inayo endelea kufanywa pia inafanywa na wananchi wa Iraq ndani au nje ya mashirika ya Ataba, miradi michache sana iliyo fanywa na watalamu wa kigeni.

Tambua kua kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu ambacho makao makuu yake yapo Najafu ni miongozi mwa vituo muhimu, kutokana na ukubwa wa kitengo hicho na wingi wa matawi yake ambayo yapo sita kila moja likiwa na idara lukuki, sehemu kilipo hivi sasa haiendani na ukubwa wa huduma kinazo toa na maendeleo kinayo piga, kwa upande mwingine hapakidhi mahitaji, ndipo Atabatu Abbasiyya ikaamua kujenga jengo maalum la kituo hicho linalo endana na utendaji wa kazi zake, kwa maelezo zaidi tembele toghuti ifuatayo: https://www.iicss.iq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: