-Tangazo- Idara ya shule za Dini za wasichana Alkafeel, imetangaza kuweka hema tatu za majira ya joto (kiangazi) kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo.

Maoni katika picha
Idara ya shule za Dini za wasichana Alkafeel chini ya ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza ratiba ya kuweka hema tatu za wanafunzi wa kike wa vyuoni katika msimu wa joto (kiangazi).

Hema la kwanza litakua katika mikoa ifuatayo: (Basra, Misaan, Dhiqaar, Muthanna) kuanzia (13 -17 Julai 2019m).

Hema la pili litakua katika mikoa ifuatayo: (Najafu, Karbala, Baabil) kuanzia (25 – 29 Julai 2019m).

Hema la tatu litakua katika mikoa ifuatayo: (Bagdad, Diyala, Diwaniyya, Waasit) kuanzia (1 - 5 Agosti 2019m).

Kila anayetaka kushiriki ajisaili kupitia mtandao wa kielektronik. Hema zitakua na ratiba zifuatazo (masomo ya dini/ familia/ malezi/ michezo/ mapumziko/ mashindano/ ziara).

Kumbuka: atakaye anza kujisajili ndiye atakaye anza kuchaguliwa.

Kwa maelezo zaidi piga simu kwa namba zifuatazo: (07707098821/ 07810116510/ 07602345585).

Au tembelea ukurasa wa shule katika mitandao ya mawasiliano ya kijamii kwa ajili ya kuangalia vigezo na kujaza fom.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: