Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limefanikiwa kumtibu bibi mwenye umri wa miaka sabini aliyekua na ugonjwa wa ajabu, kawaida moyo wa mwanaadamu hua upo upande wa kushoto, lakini moyo wa bibi huyo ulikua upande wa kulia huku mapafu na maini yakiwa upande wa kushoto.
Rais wa jopo la madaktari lililofanya upasuaji huo Dokta Haadi Khatwabi amesema kua: “Umri wa mgonjwa unakaribia miaka sabini alikua na tatizo la mchanga katika mrija wa kwenye moyo ulio sababisha kuziba kwa njia ya kusafirisha damu, kutokana na moyo wake kua upande wa kulia badala ya upande wa kushoto madaktari walishindwa kutibu tatizo lake kwa sababu vifaa tiba vilivyopo vimetengenezwa rasmi kwa kutibu matatizo ya moyo uliopo upande wa kushoto”.
Akasema kua: “Kazi ya upasuaji wa kutoa mchanga huo ilichukua saa mbili kisha mgonjwa akatoka akiwa na hali nzuri”.
Kumbuka kua mapato ya hospitali yanatumika kulipa watumishi –Ikiwa ni pamoja na mishahara ya wafanya kazi- na kusaidia wagonjwa mafakiri, sababu ya kuongezeka kwa gharama ya upasuaji inatokana na kuongezeka kwa gharama ya vifaa tiba, kuendelea na kazi kunahitaji pesa, upasuaji hufanywa na madaktari bingwa na wenye uzowefu mkubwa, ambao pia hulipwa kutokana na hela inayotolewa na mgonjwa, nao ni madaktari wa Iraq na wa kigeni.
Sehemu ya pili ya hela inayotolewa na mgonjwa husaidia kuliba mishahara ya madaktari na wauguzi, pamoja na kulipa bili za maji na umeme na mambo mengine, sambamba na kulipa tiketi, viza na bima za madaktari wa kigeni.
Kinacho baki husaidia kugharamia mradi wa (matibabu bila malipo), unao lenga kusaidia wagonjwa mafakiri na Hashdi Shaábi, na mradi wa punguzo, ambao unahusisha kuwafanyia upasuaji mafakiri kwa punguzo la bei au bila malipo kabisa.