Jumatano Asubuhi ya (8 Shawwal 1440h) sawa na (12 Juni 2019m) Atabatu Abbasiyya imefanya majlis maalum kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya ukumbi wa utawala kuomboleza kumbukumbu ya kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii tukio lililo umiza roho ya kila muumini.
Majlis hiyo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi wa Ataba pamoja na viongozi wake, mzungumzaji alikua ni Shekh Muhammad Kureitwi kutoka kitengo cha Dini, aliongelea umuhimu wa ardhi ya Baqii na utukufu wake mbele ya Mtume (s.a.w.w) pamoja na utukufu wa kuzikwa katika sehemu hiyo, kama ilivyo pokewa kutoka kwa Maimamu watakasifu (a.s), na akaeleza ubatili wa hadithi zinazo tegemewa na maadui wa Ahlulbait (a.s) wenye fikra za kiwahabi zilizo wapelekea kuvunja makaburi matakasifu katika ardhi ya Baqii, na namna zilivyo dhaifu kimapokea na kihoja.
Pia akaeleza historia ya chuki ya watu waliovunja makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s) na jinai walizo fanya, na namna walivyo vamia Karbala tukufu mwaka wa (1216h) wakaiba, wakapora na kuuwa watu, pamoja na jaribio lao la kutaka kuvamia malalo ya tukufu ya Imamu Ali (a.s) katika mji wa Najafu na jinsi wanachuoni walivyo simama imara kuwapinga.
Majlisi ikafungwa kwa kusoma mashairi na kaswida za huzuni kutokana na tukio hilo lililo umiza roho ya kila muislamu.