Kuomboleza msiba mkubwa ulio waumiza wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), tukio la kuvunjwa makaburi ya Maimamu wa Bakii (a.s) kabla ya miaka (96), baada ya Adhuhuri ya leo (8 Shawwal 1440h) sawa na (12 Juni 2019m) imefanywa maukibu (matembezi) ya pamoja kati ya watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Matembezi hayo yalianzia katika haram tukufu ya Abbasi, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walisimama kwa mistari na wakaimba kaswida zinazo amsha hisia za huzuni kutokana na tukio hilo lililoumiza roho za waumini, kisha wakaanza kutembea kuelekea katika haram ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s) kwa kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakipiga vifua vyao, walipo wasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s) wakapokewa na ndugu zao watumishi wa haram hiyo, na wakafanya majlis ya pamoja na kuimba mashairi na kaswida za huzuni, mazuwaru wote waliokua ndani ya haram wakashiriki katika majlis hiyo.
Fahamu kua siku ya mwezi nane Shawwal ni kumbukumbu ya kuvunjwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s): Imamu Hassan Almujtaba bun Amirul Mu-uminina, Imamu Ali bun Hussein Zainul-Aabidina, Imamu Muhammad bun Ali Albaaqir na Imamu Jafari Swadiq bun Imamu Baaqir (a.s), nayo ni kumbukumbu ya mwaka wa tisini na tisa (96) tangu mawahabi walipo vamia na kuvunja makaburi hayo matakatifu.