Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chazindua kifaru cha (Alkafeel/1).

Maoni katika picha
Asubuhi ya Alkhamisi (9 Shawwal 1440h) sawa na (13 Juni 2019m) imefanyika hafla ya kuzindua kifaru cha (Alkafeel/1) kilicho buniwa na kuundwa na kituo cha utafiti na uendelezaji cha kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji.

Hafla hiyo imefanywa katika mji wa mazuwaru Alqami –makao makuu ya kikosi- imehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya na naibu wake pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, na kamanda wa kikosi cha deraya cha tisa katika jeshi la Iraq na idadi kubwa ya viongozi wa jeshi la taifa na Hashdi Shaábi, bila kuwasahau viongozi wa serikali ya Karbala na wakuu wa idara.

Hafla ilifunguliwa kwa Quráni tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata ujumbe wa makamo katibu mkuu wa Ataba tukufu na mkuu wa kikosi Shekh Maitham Zaidi.

Halafu akazungumza mkuu wa baraza la mkoa wa Karbala Ustadh Naswifu Jaasim Alkhatwabi, akasifu mafanikio makubwa ya Ataba tukufu katika mambo mbalimbali.

Akaongeza kua: “leo tunasimama kujifaharisha sisi na watoto wetu na vizazi vyetu vijavyo kutokana na ushindi ulioletwa na mikono ya wananchi wa Iraq, waliotutoa katika tabaka la raia dhaifu na kuonekana kua raia shujaa na jasiri”.

Akabainisha kua: “Leo tumesimama mbele ya mafanikio mengine yanayo tokana na kazi ya mikono ya wairaq, yanayo tupa fahari kubwa kama wairaq wazalendo, ni moja ya uthibitisho wa wazi kwa maendeleo ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Halafu ikawekwa filamu inayo onyesha hatua za mradi huo, baada ya filamu hiyo wahudhuriaji wakaelekea katika uzinduzi wa (kifaru cha Alkafeel/1).

Fahamu kua kifaru cha (Alkafeel/1) kina sifa zifuatazo:

  • 1- Kina uwezo mkubwa wa kuona kupitia mitambo mbalimbali katika mazingira na nyakati zoto (mchana, usiku na wakati wa joto) kinaona umbali wa (km 14) wakati wa usiku na kinauwezo wa kutambua wa (daraja 360).
  • 2- Kimewekwa ngao za kisasa zenye uwezo mkubwa wa kuzuwia risasi.
  • 3- Kinaweza kupiga umbali wa (km4) kwa unyoofu na (km17) bila unyoofu, kina rashasha tatu kubwa ambazo unaweza kuzitumia ukiwa ndani ya kifaru, kinafanana na kifaru cha Urusi cha (D-IT).
  • 4- Kina kompyuta (computer) yenye mfumo wa kisasa wa kujihami na inaweza kufanya kazi na mifumo mbalimbali ya kujilinda sambamba na kutoa taarifa na umakini katika kulenga shabaha pia kinakwenda kwa kasi zaidi.
  • 5- Kina kiyoyozi (AC) na stoo ya chakula na sehemu ya kupumzika kwa ndani.

Kina mifumo mingine mingi ya kiusalama ambayo kijeshi haturuhusiwi kuitaja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: