Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu anaweka jiwe la msingi wa jengo la Alwafaa la kwanza kwa ajili ya kuishi familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kutokana na kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda, iliyo tolewa na Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani, Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ameweka jiwe la msingi wa jengo la Alwafaa la kwanza (Daru Ummul Banina –a.s-) kwa ajili ya kuishi familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika mji mtukufu wa Karbala, linalo jengwa katika mtaa wa Multaqa Faarisi, Alasiri ya Alkhamisi (9 Shawwal 1440h) sawa na (13/06/2019m) katika hafla iliyo hudhuriwa na watu wengi, wakiongozwa na katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu Sayyid Jafari Mussawi pamoja na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na wajumbe wa kamati za uongozi za Ataba mbili tukufu sambamba na wawakilishi wa serikali ya mkoa wa Karbala.

Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huu mtukufu ilifunguliwa kwa Quráni tukufu na Surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq halafu ukasomwa wimbo wa taifa la Iraq, ukafuata ujumbe wa makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya na kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Shekh Maitham Zaidi.

Kisha ukafuata ujumbe wa mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ambaye ni kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Halafu akazungumza Ustadh Abbasi Mussawi mwakilishi wa taasisi ya Zaharaa (a.s), ambaye alitoa shukrani nyingi kwa mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na Shekh Maitham Zaidi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, kutokana na kutilia kwao umuhimu mradi huu mtukufu na kusaidia bila kikomo.

Akabainisha kua: “Hakika mradi huu wa makazi ni sehemu ya kuonyesha fadhila ya kujitolea kwa mashahidi kwa ajili ya taifa hili”.

Mwishoni mwa hafla jiwe la msingi la jengo la Alwafaa la kwanza (Daru Ummul Banina –a.s-) la kuishi familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika mji mtukufu wa Karbala likawekwa, tunataraia litakamilika ndani ya muda uliopangwa ambao ni siku (180).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: