Vikao vya tafiti hizo vilifunguliwa kwa Quráni tukufu, na vilihudhuriwa na kundi kubwa la watafiti na wadau wa utafiti, Dokta Raidah Fayadh Al-Akili kiongozi wa vikao vya kuwasilishwa mada za kitafiti amesema kua; kulikua na mada tofauti, zoto zilikua nzuri na zenye umuhimu mkubwa, lakini matokea yalikua kama yafuatavyo:
- - Utafiti uliopata nafasi ya kwanza ni wa bibi Suzana Zain na Batuli Arandasi kutoka Lebanon, utafiti wao unasema: (Nafasi ya vyombo vya habari katika kujengo uzalendo… Iraq kama mfano).
- - Utafiti uliopata nafasi ya pili ni wa Dokta Khadija Ali Qaswiri kutoka Najafu, utafiti wake unasema (Nafasi ya nguvu ndogo katika kupambana na magaidi wa kitakfiri… Daesh wa Iraq kama mfano).
- - Utafiti uliopata nafasi ya tatu ni wa Dokta Israai Akrawi utafiti wake unasema (Maendeleo ya vyombo vya habari na athari zake kwa taifa).
Tambua kua mashindano ya tafiti mwaka huu yalikua na washiriki wengi kutoka ndani na nje ya nchi, tafiti hizi ni hazina kubwa inayo ingizwa katika maktaba zetu.