Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ametoa maelekezo ya Marjaa Dini mkuu kuhusu kumbukumbu ya siku ya fatwa ya kujilinda, ametoa maelekezo hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa ya leo (10 Shawwal 1440h) sawa na (14 Juni 2019), iliyo swaliwa ndani ya haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s).
Enyi mabwana na mabibi… nakusomeeni ujumbe maalum kutoka katika ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu kuhusu kumbukumbu ya fatwa ya kujilinda ya wajibu kifaya.
Katika siku kama ya jana tarehe kumi na tatu Juni mwaka (2014m) – miaka mitano iliyo pita- Marjaa Dini mkuu alitoa wito wa fatwa yake tukufu ya wajibu kifaya wa kujilinda mahala hapa, aliwaomba wairaq wenye uwezo wa kubeba siraha walisaidie jeshi la serikali kuilinda Iraq na raia wake pamoja na maeneo matakatifu dhidi ya magaidi wa Daesh, waliokua wameteka eneo kubwa na idadi kadhaa ya mikoa na wakawa wanatishia kuteka mji mkuu wa Bagdad pamoja na mikoa mingine pia, raia wa Iraq wazee kwa vijana kutoka jamii tofauti wakajitokeza na kuingia katika uwanja wa vita wakiwa na hamasa kubwa na ujasiri usiokua na kifani, wakapigana vita kali sana kwa muda wa miaka mitatu, wakaonyesha ushujaa wa hali ya juu, katika vita hiyo walijitolea maelfu ya mashahidi na majeruhi kwa ajili ya kuokoa taifa lao tukufu na kulinda heshima na maeneo matakatifu, hadi Mwenyezi Mungu alipo wapa ushindi na kuwawezesha kumuondoa adui katika ardhi alizo kua ameziteka na kuangamiza kabisa utawala wao wa kigaidi.
Usingepatikana ushindi huo mkubwa kama sio kuwepo kwa mshikamano na umoja wa wairaq, hata vyama vya kisiasa viliweka pembeni tofauti zao na mizozo yao, pamoja na kulinda maslahi binafsi na ya vyama vyao na wakatanguliza maslahi ya taifa na wananchi, sambamba na ushirikiano tuliopewa na nchi rafiki zilizo jitolea kuisaidia Iraq katika mapambano dhidi ya magaidi wa Daesh.
Baada ya vita kuisha na kupatikana ushindi wa wazi kwa kukomboa miji mbalimbali iliyokua imetekwa na magaidi wa Daesh tofauti zimerudi upya, -tena waziwazi- watu ambao waliungana wakashikamana na kupigana pamoja dhidi ya adui wao Daesh, leo wametofautiana kila mmoja anaangalia maslahi yake, na wanashambuliana kwenye majukwaa na mitandao ya mawasiliano ya kijamii, -miongoni mwa wanao onyesha kuto elewana ni wizara ya ulinzi na ya mambo ya ndani- bado ufisadi unaendelea katika taasisi za serikali, hakuna utemdaji wa wazi wala mafisadi hawaja wajibishwa, bado tunashuhudia matatizo ya kiutawala, ukosefu wa ajira na upungufu mkubwa katika huduma za msingi –ukiacha marekebisho yaliyo fanyika hivi karibuni katika baadhi ya huduma hizo- yote hayo yanasababisha ugumu wa maisha ya wananchi, bado mambo yaliyo sababisha mwanya wa kujipenyeza magaidi hayajarekebishwa, ambayo ni hatari kwa taifa, uhasama umeongezeka baada ya kutulia kwa muda wakati ambao kila mtu alikua anajishughulisha na vita dhidi ya Daesh.
Kuendelea kupigania vyeo na mali ni kuamsha matatizo ya kiusalama, kikabila na kuchochea ubaguzi, na kunachelewesha ujenzi wa maeneo yaliyo athirika na vita, pia ni kuwapa nafasi mabaki ya magaidi wa Daesh ya kuendelea kufanya jinai zao na kuvuruga amani na utulivu wa taifa, wanaweza kupata hadi hifadhi kwa baadhi wa makundi yanayo hasimiana na hapo mambo yakawa mabaya zaidi.
Ili kurudisha utulivu na amani kwa wananchi na kuwafanya waishi vizuri inahitajika kuacha kuvunja sheria na kumpa kila mtu haki ya kuishi kwa uhuru na amani, bila kufanya hivyo inakua ni sababbu ya kulirudisha taifa katika machungu yasiyo sahaulika.
Wahusika wanatakiwa kua makini na kuchukua tahadhari kubwa ya kutofanya mambo yanayo weza kuturudisha katika matatizo, washirikiane kwa nia moja kumaliza matatizo, sambamba na kupewa ushirikiano maalum na maafisa usalama katika kuharibu kila njama ya ugaidi itakayo pangwa kabla ya kutekelezwa, ulinzi uimarishwe kwenye maeneo yote yanayo hisiwa kutumiwa na magaidi kuanzisha harakati zao, hairuhusiwi kufumbiwa macho swala hili kwa namna yeyote ile.
Salam za unyenyekevu na heshima kubwa ziwafikie mashahidi watukufu, na wapenzi zetu katika familia zao, pamoja na ndugu zetu wapiganai walio jeruhiwa na waliopata ulemavu, na wapiganaji watukufu wa vikosi vyote wanao kesha kwa ajili ya kulinda taifa na wananchi watukufu… tunamuomba Mwenyezi Mungu awalinde na awape nguvu, na sote kwa ujumla atujalie kila lenye kheri kwetu na kwa taifa letu hakika yeye ni mwingi wa rehema mwenye kurehemu.