Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinatangaza kufanyika kwa kongamano la pili kwa wanafunzi wa sekondari kuanzia tarehe: 18 hadi 22 Julai 2019m.
Na kongamano la tatu kwa wanafunzi wa sekondari litafanyika tarehe: 25 hadi 29 Septemba 2019m.
Fahamu kua kongamano hili linahusu wanafunzi wenye umri kati ya miaka (13 – 18) kutoka mkoa wa Karbala na litakua na: (masomo ya kitamaduni, kifamilia, kimaadili, kiufundi -kujifunza kazi za mikono-, mijadala, mashindano na matembezi).
Kwa yeyote anayependa kujisajiri afike kwenye ofisi za kituo cha utamaduni wa kifamilia zilizopo Karbala/ mtaa wa Mulhaqu/ jengo la Swidiiqah Twahirah (a.s)/ ghorofa ya tano kujaza fomu maalum ya kujisajili.
Tambua: Usafiri wa kwenda na kurudi upo, kwa maelezo zaidi piga simu namba: 07828884555.