Kwa kuhudhuria viongozi wa Dini na wa kitamaduni pamoja na kundi kubwa la wakufunzi na watafiti kutoka miji ya Ulaya, Adhuhuri ya Jumapili (16/06/2019m) sawa na (12 Shawwal 1440h) mji mkuu wa Ujerumani Balin imefungwa warsha ya kielimu kuhusu (Nafasi ya Dini katika kueneza Amani), mwakilishi wa jumuwiya za Ulaya na kutambuana kwa Dini “Mwana habari Alaa Khatibu”aliwasilisha ujumbe wa mwisho kwa kusema kua: Tuna amini katika kueneza utamaduni wa Amani na kuachana na utamaduni wa chuki na ubaguzi, tunaungana na taasisi zinazo himiza watu wote kuishi kwa Amani, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa mbele ya watu walio uwawa na magaidi, chini ya usimamizi wa Mheshimiwa Sayyid Hussein Ismail Swadri pamoja na ushirikiano wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani na jumuwiya za Ulaya za kutambuana kwa Dini, tumefanya kongamano la amani katika mji mkuu wa Ujerumani Balin (15 -16 Juni 2019m) na kufanya kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu kufanyika kwa mauwaji ya Spaika, wameshiriki viongozi wa Dini, wanasiasa, waandishi wa habari na wengineo wa jinsia tofauti na wawakilishi wa taasisi za kiraia kutoka nchi tofauti duniani.
Akaongeza kua: Washiriki wametoka na maazimio yafuatayo:
Kwanza: Tunaziomba nchi mbalimbali na taasisi za kimataifa pamoja na umoja wa Ulaya na umoja wa mataifa kuchukua jukumu lao la kibinaadamu la kuzuwia vitendo vya kigaidi na kufunga vyanzo vyao vya kifikra na kiuchumi.
Pili: Kufuatilia jinai ya mauwaji ya Spaika na kuyaingiza katika orodha ya mauwaji ya kimbali (halaiki) pamoja na kuwakamata watu wote walio husika na mauwaji hayo na kuwafikisha katika vyombo vya sharia.
Tatu: Kueneza utamaduni wa kuishi kwa Amani kwa kufanya makongamano ya kutambuana baina ya Dini tofauti.
Nne: Kusaidia matokeo chanya ya Maraajii Dini wenye mafundisho yanayo himiza Amani.
Tano: Umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana kwa taasisi za kiraia na kidini mashariki na magharibi.
Sita: Umuhimu wa vyombo vya habari kukumbusha misingi ya kusameheana na kupendana na kuachana na chuki na uhasama.
Mwisho: Tunatoa shukrani kwa taasisi ya mambo ya nje ya Ujerumani na taasisi za utafiti wa mambo ya sekula hapa Ujerumani na kila aliye changia kufanikisha mkutano huu.