(Nafasi ya Dini katika kueneza Amani) warsha ya kielimu jijini Balin Ujerumani

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya wiki ya Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya Jumapili (16/06/2019m) sawa na (12 Shawwal 1440h) mji mkuu wa Ujerumani Balin imefanyika warsha ya kielimu iliyo hudhuriwa na wawakilishi wa Atabatu Husseiniyya na wasomi wengine bila kuwasahau viongozi wa hauza kuhusu (Nafasi ya Dini katika kueneza Amani).

Warsha ilifunguliwa kwa kuwasilishwa mada mbalimbali na kujadili mambo tofauti, ujumbe wa kwanza uliwasilishwa na mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika nchi za Ulaya Sayyid Ahmadi Radhi, ambaye alisema kua: (Nawatakia Amani wapenzi watukufu mlio itikia mwaliko wetu…).

Ukafuata ujumbe wa balozi wa Iraq nchini Ujerumani “Dokta Dhiyaau Dabbasi” akasema kua: (Nifuraha kubwa hapa Balin kuwapokea viongozi wa Dini na wanachuoni kutoka Iraq, ni fahari kubwa na ushahidi wa wazi kua Iraq ni kitovu cha utamaduni cha tangu zamani, pamoja na mazingira magumu iliyo pitia na bado inapitia inaendelea kupitia mazingira magumu, lakini imeendelea kua nuru inayo angazia binaadamu wa sasa na wajao…).

Kisha zikafuata mada za kujadiliwa, mada ya kwanza ilikua inasema: (Nafasi ya Dini katika kueneza Amani) iliyo wasilishwa na Mheshimiwa Shekh Qadhi Muhammad Kan’ani rais wa mahakama za Jafariyya nchini Lebanon.

Mada ya pili na yamwisho ilikua ya Dokta Swahibu Naswaar isemayo (Amani katika Dini tatu, Uyahudi, Ukristo na Uislamu).

Kikao kilipambwa na maoni mbalimbali kutoka kwa washiriki, pamoja na maswali yaliyo jibiwa na watoa mada na wakafafanua zaidi sehemu zilizo hitaji ufafanuzi.

Mwisho midani na zawadi zikagawiwa kwa washiriki wa warsha hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: