Kituo cha utamaduni wa familia kimefungua warsha elekezi ya kubaini changamoto na kuzitafutia utatuzi

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa mikakati ya kutatua matatizo ya kijamii, kimeanza kutoa mafunzo kwa makundi tofauti ya wanajamii, kwa kuwapa mihadhara mbalimbali ya kimaadili kina mama wa mji mtukufu wa Karbala.

Unatolewa mhadhara mmoja kila wiki chini ya anuani isemayo: (Changamoto za kinafsi na kimaadili na njia za utatuzi wake) chini ya wakufunzi walio bobea katika sekta hiyo, na wenye uwezo mkubwa wa kutatua changamoto mbalimbali.

Kituo kimetoa wito kwa yeyote anayependa kushiriki katika program hii wapige simu namba (07828884555) au awasiliane nasi kupitia (Viber, WhatsApp na Telegram) kwa maelezo zaidi ingia katika linki ya kituo cha utamaduni wa familia ifuatayo: https://t.me/thaqafaasria1

tambua kua usafiri wa kwenda na kurudi umeandaliwa na kituo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: