Kutoka Karbala… Vikosi vya Hashdi Shaábi vinaadhimisha mwaka wa tano tangu kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda kwa kuwakumbuka mashahidi wao kupitia matembezi makubwa

Maoni katika picha
Vikosi vya Hashdi Shaábi katika mji wa Karbala vimefanya matembezi waliyo yapa jina la (Alwafaa) katika kuadhimisha mwaka wa tano tangu Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu Sayyid Ali Husseini Sistani alipo toa fatwa tukufu ya kujilinda dhidi ya magaidi wa Daesh na kukomboa ardhi ya Iraq iliyokua imetekwa na magaidi hao.

Matembezi hayo yamefanyika katika mji wa Karbala kwenye eneo la katikati ya haram mbili tukufu kwa ushiriki wa kikosi cha Abbasi (a.s) blugedi ya (26 Hashdi Shaábi) pamoja na vikosi vingine, kikiwemo kikosi maalum cha Furaat Ausatu, huku wamenyanyua picha za mashahidi walio uwawa kwa ajili ya ukombozi wa taifa hili, walijitolea nafsi zao kwa ajili ya kulinda utukufu na heshima ya taifa, katika matembezi hayo zimeimbwa kaswida na kutolewa matamko mbalimbali na viongozi wa Hashdi Shaábi.

Kuhusu matembezi hayo tumeongea na mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Shekh Maitham Zaidi amesema kua: Hakika matembezi yanavipengele tofauti ikiwa ni pamoja na uimbaji wa kaswida na matamko ya viongozi wa Hashdi Shaábi katika kuadhimisha fatwa na umuhimu wake katika kulinda taifa, sambamba na kukumbuka damu za mashahidi na majeruhi pamoja na namna raia wa Iraq kwa ujumla walivyo pambana kukomboa taifa lao tukufu, tunamuomba Mwenyezi Mungu awadumishe Maraajii wetu watukufu na atuwezeshe daiama kukubali wito wao na kutii maagizo yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: