Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya yatoa masomo ya ziada (twishen) kwa wanafunzi wanao karibia kuhitimu

Maoni katika picha
Katika kusaidia safari ya elimu na malezi na kutokana na kukaribia kwa mitihani ya mwisho wa mwaka, kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu na kujiandaa na mitihani hiyo, Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya, imeandaa twisheni za bure kwa wanafunzi wa kidato cha tatu, katika ofisi za makao makuu ya tawi hilo kwenye wilaya ya Hindiyya.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa tawi la Maahadi Sayyid Haamid Mar’abi amesema kua: “Twisheni hizi ni fursa ya kutumia vizuri kipindi cha likizo na kujiandaa kufanya mitihani ya mwisho wa mwaka, kuna idadi kubwa ya wanafunzi ambao hawana uwezo wa kujiunga na twisheni za kulipia, kwa hiyo twisheni hizi ni muhimu sana kwao”.

Akaongeza kusema kua: “Tawi la Maahadi baada ya kukamilisha maandalizi yote muhimu limewasiliana na walimu wazowefu kwa ajili ya kufundisha mada zifuatazo: (Maarifa ya Qur’ani, Lugha ya kiarabu, Fizikia, Kemia, Hesabu na Kiengereza), wanafunzi wote walio omba kushiriki katika semina hizo watapewa mtihani wa majaribio”.

Akasisitiza kua: “Twisheni hizi zimekua na mwitikio mkubwa, na wanafunzi wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na walimu walio jitolea kuwafundisha tena kwa ustadi mkubwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: