Maoni katika picha
Ameyasema hayo alipo tembelea miradi ya Ataba akiwa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi.
Akaongeza kusema kua: “Sisi tunaunga mkono kwa nguvu zote miradi hiyo, ziara yetu hii ni uthibitisho wa kukubaliana na miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Wametembelea jengo la Saqaa/2 katika eneo la Ibrahimiyya ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, jengo lenyo miradi mingi ya Ataba, ukiwemo mradi wa Darul-Kafeel ya uchapaji na usambazaji wa vitabu, kiwanda cha maziwa ya Alkafeel chini ya shirika la Nurul-Kafeel la bidhaa za vyakula, kisha wakatembelea kituo cha Ataba tukufu cha kuegesha magari, kiongozi wa ofisi za Ataba amesifu maendeleo mazuri ya miradi ya Ataba na namna inavyo saidia jamii ya wananchi wa Iraq, akapongeza kazi nzuri ya kufanikiwa miradi hiyo.
Kabla ya matembezi hayo walimzuru Abulfadhil Abbasi (a.s) na wakatembea korido za haram hiyo tukufu kuangalia maendeleo ya Ataba tukufu katika sekta tofauti za kiutamaduni, kielimu na kiutumishi.