Najafu yashuhudia ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (3500) katika mradi wa semina za Qur’ani

Maoni katika picha
Mkoa wa Najafu umeshuhudia zaidi ya wanafunzi (3500) katika mradi wa semina za Qur’ani za kipindi cha majira ya joto (kiangazi), zinazo simamiwa na tawi la Maahadi ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya katika mji wa Najafu, wamekaa katika misikiti na husseiniyya tofauti.

Mradi huu unafanywa katika miji tofauti, wakazi wa Najafu wamejitokeza kwa wingi kuandikisha watoto wao, katika semina hizi hufundishwa (Qur’ani tukufu, Adida, Fiqhi, Akhlaqi na Sira), sambamba na masomo mengine ya kimalezi, kwa lengo la kukazia maarifa ya dini katika nafsi za vijana hao.

Shekh Jawadi Nasrawi mkuu wa Maahadi amesema kua: “Mradi huu unalenga kuandaa kizazi kinacho fuata mafundisho ya vizito viwili Qur’ani na kizazi kitakatifu, idadi ya washiriki inaongezeka mwaka baada ya mwaka”.

Akaongeza kua: “Tumeandaa kila kinacho hitajika kwa wanafunzi, pamoja na vivutio mbalimbali vinavyo endana na umri wao, kuna utaratibu mzuri wa kusafirisha wanafunzi kutoka majumbani kwao hadi sehemu za masomo kila siku asubuhi na kuwarudisha baada ya kumaliza ratiba za masomo”.

Kumbuka kua mradi huu ni miongoni mwa miradi muhimu katika Maahadi ya Qur’ani tukufu, kutokana na umuhimu wake kitamaduni na kidini kwa vijana, pia ni namna bora ya kutumia kipindi cha likizo za kiangazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: