Kwa juzu hamsini na nne Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa kitabu cha kwanza kikubwa kuhusu fatwa takatifu ya kujilinda

Maoni katika picha
Kutokana na umuhimu wa fatwa tukufu iliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu kwa ajili ya kuilinda Iraq na maeneo matakatifu, na kufuatia kuadhimisha mwaka wa tano tangu kutolewa kwa fatwa hiyo, Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa kitabu kikubwa cha kwanza kuhusu fatwa ya kujilinda iliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani, iliyo pata mwitikio mkubwa kutoka kwa raia wa Iraq walio jitokeza kwa wingi kujiunga katika vikundi vya wapiganaji dhidi ya magaidi wa Daesh.

Kuhusu kitabu hicho tumeongea na makamo rais wa kitengo cha habari na utamaduni Mhandisi Ahmadi Swadiq Hassan amesema kua: kutokana na maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na ufuatiliaji wa karibu wa Sayyid Liith Mussawi pamoja na baraka za Mwenyezi Mungu bila kusahau baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha kitabu kinacho elezea fatwa tukufu ya kujilinda pamoja na mambo yaliyo tokea baada ya fatwa hiyo ikiwa ni pamoja na mwitikio wa raia wa Iraq na namna walivyo toka makundi kwa makundi kwa ajili ya kulinda taifa lao.

Akaongeza kua: kitabu hiki kinajuzu hamsini na nne, kimeandika kuanzia pale fatwa ilipo tolewa ndani ya haram ya Husseiniyya kupitia ulimi wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai pamoja na mwitikio wa wairaq na matukio mengine yakiwemo mapigano mbalimbali ya kukomboa miji ya Iraq na kuundwa kwa vikosi vya kusaidia wakimbizi.

Akaendelea kusema: kitabu hicho kimeeleza pia nafasi ya Ataba tukufu na hauza za kielimu pamoja na taasisi za serikali na zisizokua za serikali namna zilivyo unga mkono fatwa hiyo, miongoni mwa taasisi hizo ni ile ya Ain pamoja na namna mawakibu Husseiniyya zilivyo simama imara kusaidia wapiganaji pamoja na wakimbizi.

Akabainisha kua: katika kitabu hicho tumeandika pia nafasi ya vyombo vya habari katika vita, namna vilivyo kua vikiripoti matukio ya kivita katikati ya vita, walikua pamoja na vikosi vya wapiganaji pia walikua pamoja na vikosi vya uokozi na kutoa misaada, mambo yote hayo yameandikwa katika kitabu hicho tena kwa umakini mkubwa ili kutunza kumbukumbu hiyo kwa vizazi vijavyo, wasome na kujua kua Iraq ilikaribia kuangamia wakajitokeza watu kuikomboa kupitia fatwa hiyo takatifu.

Fahamu kua kazi ya kuandika kitabu hiki ilihitaji muda na umakini mkubwa ili kukifanya kiendane na tukio hili tukufu la kihistoria pia kiendane na heshima ya Marjaa Dini mkuu pamoja na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: