Dondoo za kumbukumbu ya: mwezi kumi na tano Shawwal ni kumbukumbu ya kifo cha bwana wa mashahidi Ammi wa Mtume Hamza bun Abdulmutwalib (a.s).

Maoni katika picha
Hamza bun Abdulmutwalib Alhashimiy Alquraishiy, ni swahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ammi yake, na ndugu yake kwa kunyonya pia ni mmoja wa mawaziri wake kumi na nne, alikua Ammi bora zaidi kwake, kutokana na kauli yake isemayo: “Mbora wa ndugu zangu ni Ali, na mbora wa Ammi zangu ni Hamza”.

Alikua anamzidi Mtume Muhammad (s.a.w.w) miaka miwili, alikua na ukaribu nae upande wa mama yake, mama yake anaitwa Hala binti Wahibu bun Abdulmanafi, mtoto wa Ammi yake na Amina binti Wahabi bun Abdulmanafi mama wa Mtume Muhammad. Alipewa jina la bwana wa mashahidi (Sayyid Shuhadaa), Simba wa Mwenyezi Mungu na Simba wa Mtume, jina la kuniya anaitwa Abu Ammaarah, na inasemekana anaitwa Abu Ya’ala. Hamza alikua kijana shujaa mkarimu na mpole, alikua shupavu zaidi katika vijana wa kikuraishi, katika zama za ujinga alishuhudia vita ya Fujaar kati ya kabila la Kinana na Qaisi.

Alisilimu mwaka wa pili wa Utume, baada ya kusilimu kwake makuraishi wakatambua kua Mtume Muhammad amepata nguvu na kwamba Hamza atamlinda, wakapunguza kumfanyia baadhi ya maudhi waliyo kua wanamfanyia, kisha Hamza alihamia Madina, Mtume (s.a.w.w) akaunga undugu baina yake na Zaidi bun Haarith. Alikua kamanda wa kwanza kuteuliwa na Mtume Muhammad, alipigana vita ya Badri na akamuua Shaiba katika mapambano ya mmoja mmoja (mubaraza) kisha akauwa washirikina wengine wengi, alipigana pia katika vita ya Uhudi mwaka wa tatu hijiriyya, kabla ya kuuwawa kwake alikua amesha wauwa washirikina thelathini na moja.

Aliye muuwa alikua ni Wahshi bun Harbi Alhabashiy kijana wa Jubair bun Mutwi’im, washirikina waliusulubu mwili wake, Hindu binti Utba aliamuru apasuliwe tumbo na akatoa ini lake, akataka kulila lakini hakuliweza akalitema, Mtume (s.a.w.w) akasema: “Kama angelimeza na kuingia tumboni mwake asingeguswa na moto”, Mtume akaenda kumtafuta Hamza, akamtuka katikati ya jangwa akiwa amepasuliwa tumbo, jambo hilo lilimuumiza sana, akasema: “Mwenyezi Mungu akurehemu ewe Ammi yangu, ulikua muunga undugu na mtenda mema”. Hamza akazikwa pamoja na mtoto wa dada yake Abdullahi bun Jahashi.

Pakisemwa “simba wa Mwenyezi Mungu” akili ya msikiliza huenda moja kwa moja kwa kamanda huyu mujaahid Hamza bun Abdulmutwalib bun Hashim bun Abdulmanafi bun Quswai bun Kilabi jemedari jasiri Abu Ammaarah Alkuraishiy Alhashimiy Almakkiy, kisha Almadaniy, Albadriy Ashahiid, Ammi wa Mtume (s.a.w.w) na ndugu yake kwa nyonya, Hamza anautukufu mkubwa sana unafaa kuandikwa kwa wino wa dhahabu, historia imeandika utukufu wake kwa nuru na umetunzwa kwa vizazi na vizazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: