Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeweka mazingira mazuri kwa wanafunzi wakati wa kufanya mitihani ya mwisho

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kua kimeweka mazingira mazuri ya kufanya mitihani kwa wanafunzi wa (Udaktari – Udaktari wa meno – Uuguzi) wanao tarajiwa kufanya mitihani ya kuhitimu masomo, huu ni mwendelezo wa utaratibu wake kwa wanafunzi wa sekula, kwa kufuata utaratibu wa kisasa unao tumiwa na vyuo vikuu ndani na nje ya Iraq.

Kila kitivo kimeandaliwa ukumbi wake wa mitihani na kuwekwa kila kitu kinacho hitajiwa na mwanafunzi, ili waweze kufanya mitihani kwa amani na utulivu, chini ya utaratibu uliotolewa na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, uongozi wa chuo umekua ukifanya ukaguzi katika kumbi hizo kila wakati.

Kumbuka kua Chuo kikuu cha Al-Ameed ni taasisi ya kielimu ambayo ipo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu inayo tambuliwa na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, kilifungua kitivo cha kwanza cha udaktari, na kinatarajiwa kua kitovu cha elimu, kinatumia selebasi ya kimataifa inayo kiwezesha kuingia katika orodha ya vyuo vikuu tegemezi, chuo hicho kipo katika mkoa mtukufu wa Karbala mwanzoni mwa barabara ya (Karbala – Najafu) karibu na nguzo namba (1238).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: