Asilimia %96 ya mafanikio ndani ya miaka mitatu na nusu: Jumla ya upasuaji 409 wa moyo wazi umefanywa katika hospitali ya Alkafeel.

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza jumla ya upasuaji (409) wa tatizo la moyo wazi uliofanywa na madaktari wazalendo na wakigeni imefanikiwa kwa asilimia (%96).

Mkuu wa hospitali Dokta Jaasim Ibrahim amesema kua: “Upasuaji umefanywa na madaktari bingwa wa kiiraq na kigeni kwa watoto na wakubwa, mafanikio yaliyo patikana yanatokana na uhodari wa madaktari, wauguzi na vifaa tiba vya kisasa vilivyopo”.

Akasisitiza kua: “Msukumo mkubwa wa kupatikana kwa mafanikio haya ni kufanya kazi kwa tim na kwa moyo wa kujitolea, mambo ambayo ndio sifa kubwa ya watumishi wetu na hiyo ndio fahari yetu”.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel tembelea toghuti ya hospitali ifuatayo: (www.kh.iq) au piga simu namba: (07602344444 au 07602329999).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: