Maandalizi ya mwisho: Kamati inayo andaa kongamano la kwanza la kimataifa kuhusu turathi za Karbala inafanya kikao cha kushauriana.

Maoni katika picha
Maandalizi ya mwisho na kuangalia yaliyo azimiwa na kikao kilicho pita, kamati kuu ya maandalizi ya kongamano la kimataifa la kwanza kuhusu turathi za Karbala litakalo fanywa chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu/ kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika kituo cha turathi za Karbala, chini ya kauli mbiu isemayo: (Turathi zetu ni utambulisho wetu) na anuani isemayo: (Turathi za Karbala na nafasi yake katika maktaba za kiislamu) kuanzia tarehe (7 – 8 Novemba 2019m) sawa na (10 – 11 Ribiul-Awwal 1441h), wamefanya kikao cha kushauriana kilicho ongozwa na rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu Shekh Ammaar Hilali na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Kikao hicho kilikua kinaangalia maazimio yaliyo fikiwa katika kikao kilicho pita, na kukagua utendaji wa kamati ndogondogo za maandalizi, pamoja na kujadili uwezekano wa kuwa na toleo maalumu la kitabu kuhusu kongamano hilo, kitakacho pewa washiriki wa kongamano.

Miongoni mwa mambo yaliyo pasishwa na mkutano huo ni kujitambulisha kwa baadhi ya wanachuoni wakubwa ndani na nje ya Iraq, pamoja na kufungua milango ya kupokea tafiti mbalimbali na kuzishindanisha ili kupata zitakazo wasilishwa kwenye kongamano na kuweka utaratibu maalum wa jambo hilo.

Kumbuka kua kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu imetoa wito kwa watafiti na wasomi washiriki kuandaa mada za kitafiti kwa kufuata maelekezo yaliyopo katika linki ifuatazo:

https://alkafeel.net/ar-news/index?id=8638
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: