Kwa mahudhurio makubwa: Kituo cha utamaduni wa familia chafanya warsha ya pili ya kubaini changamoto za makuzi (murahaqa) na utatuzi wake.

Maoni katika picha
Wiki ya pili mfululizo kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea na warsha za malezi na mambo ya kinafsi kwa kina mama, kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto za makuzi (murahaqa).

Kiongozi wa kituo tajwa hapo juu Ustadhat Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kwa sifa za Mwenyezi Mungu na usaidizi wake pamoja na Baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), bado tunaendelea na ratiba yetu inayokusudia kujenga uwelewa kwa wakina mama wa namna ya kuamiliana na makuzi ya watoto wao, warsha ilikua na sehemu mbili, kwanza (Changamoto za makuzi na utatuzi wake) na sehemu ya pili ilihusu (Namna gani utamfanya kijana ajiamini?), mada tofauti zimewasilishwa katika warsha hiyo zinazo endana na mazingira halisi tunayo ishi sambamba na kueleza ufumbuzi wa changamoto mbalimbali”.

Akaongeza kua: “Hali kadhalika kulikua na maswali pamoja na kupokea ushauri na maoni ya washiriki”.

Akasisitiza kua: “Tumeona kuna mwitikio mkubwa na tumepata mahudhurio mazuri, kutokana na mada zilizo wasilishwa kukata kiu ya washiriki”.

Fahamu kua warsha hii ni sehemu ya harakati za kituo na zinasimamiwa na jopo la wataalamu wa sekta ya malezi wenye uwezo wa kupambana na changamoto yeyote katika sekta hiyo”.

Kumbuka kua kituo kilikua kimesha toa mialiko ya kushiriki katika warsha hii kupitia simu (07828884555) au mitandao ya kijamii (Viber, Whatsapp, Telegram), au kwa kutumia linki ifuatayo: https://t.me/thaqafaasria1 tambua kua usafiri wa kwenda na kurudi umeandaliwa na kituo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: