Uongozi wa hospitali ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu tangu kufunguliwa kwake, imekua ikiwapa kipaombele majeruhi wa vita ya kukomboa ardhi ya Iraq iliyokua imetekwa na magaidi wa Daesh, sawa majeruhi hao wawe ni katika wanajeshi wa serikali au Hashdi Shaábi, wamekua wakipewa matibabu ya aina yeyote yanayo hitajika.
Hospitali imetangaza kua imetoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa Elfu kumi mia mbili themanini na tisa wa Hashdi Shaábi ndani ya miaka mitatu, na bado inaendelea kutoa huduma huzo ambazo zimejumuisha na familia za mashahidi na majeruhi.
Mkuu wa hospitali Dokta Jaasim Ibrahimi amesema kua: “Hakika hospitali imewapa umuhimu zaidi kwa kuwapima na kuwatibu bure majeruhi wa Hashdi Shaábi, hili ni jambo moja tunalo weza kuwafanyia makamanda waliojitolea damu zao kwa ajili ya kulinda taifa la Iraq lisinajisiwe na magaidi”.
Akabainisha kua: “Ndani ya miaka mitatu, tumetoa zaidi ya bilioni tano dinari za Iraq kwa ajili ya kuwatibu mafakiri na watu wasiokua na uwezo, ambao tumewafikia kupitia mradi wa (matibabu bila malipo) mradi huo unasaidiwa na ofisi za Maraajii, taasisi za kibinaadamu pamoja na mitandao ya mawasiliano ya kijamii, na hulazimika kuwatibu na kuwagharamia wagonjwa hao baada ya kuwaleta kwenye hospitali ya Alkafeel kutoka katika miji yao”.
Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel tangu ilipotolewa fatwa tukufu ya kujilinda na kulinda maeneo matakatifu ni sawa na taasisi zingine za Atabatu Abbasiyya, imefanya kila iwezalo kuwasaidia wapiganaji waliopata majeraha na kujaribu kupunguza maumivu yao, kutokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu yanayo himiza jambo hilo, pia ni sehemu ya wajibu wake kwa majeruhi, imebeba pia jukumu la kuwanunulia viungo bandia wale waliopoteza viungo vyao.