Waziri wa utamaduni na athari: Anazingatia kuimarisha uhusiano na Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya umetembelea wizara ya utamaduni na utalii ya Iraq na kukutana na waziri Dokta Abdul-Amiir Hamdani ofisini kwake mjini Bagdad, pande zote mbili zimezungumzia umuhimu wa kuimarisha uhusiano baina ya Atabatu Abbasiyya na wizara katika kuboresha utendaji na kulinda nakala kale sambamba na kutunza filamu za mambo ya kale.

Waziri wa utamaduni na utalii Dokta Abdul-Amiir Hamdani katika kikao cha pamoja na mjumbe wa idara yake Dokta Abbasi Rashidi Mussawi na rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nuris Dahani pamoja na msanii wa filamu Azhar Khamisi kutoka kituo cha uzalishai Alkafeel, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika sekta ya vielelezo vya namba pamoja na kutoa ushirikiano kwa wale wanaofanya utafiti wa shahada ya udokta (digrii ya tatu) na masta (digrii ya pili) kwa kufuata kanuni za hati miliki ya fikra, pia Hamdani amezungumza kuhusu filamu za Atabatu Abbasiyya tukufu.

Akatoa wito kwa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu kufanya utafiti wa zama za ufalme na zama za jamhuri kupitia vielelezo vilivyopo chini ya wizara.

Wageni kutoka Atabatu Abbasiyya wakaonyesha ushahidi wa wakfu zilizo tolewa na utawala uliopita kwa Ataba tukufu mwaka 1991m bila kufuata sharia, wizara ilikua imesha ahidi kutoa ushirikiano katika swala hilo kupitia ziara aliyofanya Dokta Hamdani katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mkoa wa Karbala wiki iliyopita.

Tambua kua ziara hii imefanyika baada ya ziara ya waziri wa utamaduni na utalii Dokta Abdul-Amiir Hamdani katika Atabatu Abbasiyya siku chache zilizo pita, lengo la ziara hii ni kuimarisha ushirikiano baina ya pande mbili kwa maslahi ya taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: