Maandalizi ya safari ya washiriki wa ushindi na mawakibu za kutoa misaada bado yanaendelea

Maoni katika picha
Mawakibu za kutoa misada ya kimkakati zilizo chini ya idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu bado zinaendelea na maandalizi ya kushiriki katika matembezi makubwa yatakayo fanyika Ijumaa (28 Juni 2019m) katika mkoa wa Karbala, matembezi ya kuhuisha utiifu kwa Marjaa Dini mkuu na kuahidi kua pamoja naye kwenye kila jambo, sambamba na kuadhimisha kumbukumbu ya fatwa tukufu ya kujilinda iliyo tolewa katika siku kama hizi mwaka wa (2014m) na kua sababu ya kuhifadhika ardhi ya Iraq na maeneo matakatifu, kwa utukufu wake na mwitikio wa wananchi wa Iraq ukapatikana ushindi mkubwa, magaidi wa Daesh wakapigwa na ardhi ya Iraq ikakombolewa.

Kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu hii kwa namna nzuri inayo endana na utukufu wake, kimefanyika kikao kwenye jongo la Alqami kujadili maandalizi, kikao hicho kimemuhusisha Shekh Abbasi Akaaishi kiongozi wa idara zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya kwenye mikoa (12) akaeleza hatua ya mwisho iliyo fikiwa katika maandalizi ya matembezi hayo pamoja na kujadili mambo mengine kuhusu shughuli za idara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: