Kamati inayo simamia shindano hilo ilipokea idadi kubwa ya visa kutoka kwa washiliki ndani na nje ya mkoa wa Karbala, kwa mujibu wa mada zilizokua zikishindaniwa na kanuni zake, na walioibuka washinzi ni:
- - Sara Muhammad Ali, kisa kisemacho (katika bustani ya babu kuna tandiko).
- - Hussein Ali Rahiif, kisa kisemacho (kujitolea tende).
- - Dhuha Ridhwa, kisa kisemacho (kule kila kitu ni kizuli).
- - Swadiq Mahadi Hassan, kisa kisemacho (Amani ya rafiki zangu).
- - Suzana Abdullahi, kisa kisemacho (zawadi).
Kumbuka kua shindano hili lilikua na masharti yafuatayo:
- 1- Kisa kufuate kanuni za kiuandishi na maadili ya watoto.
- 2- Kielezee ujasiri wa eshi la Iraq na Hashdi Shaábi kwa ujumla bila (kumlenga mtu maalum) namna walivyo pambana kulinda taifa na maeneo matakatifu.
- 3- Kisiwe kimesha wahi kuandikwa au kutolewa siku za nyuma kupitia nyaraka au mitandao ya kielektronik.
Kamati imesema kua visa vitano vilivyo shinda vitachapishwa kwa gharama za Atabatu Abbasiyya na waandishi wa visa hivyo watapewa zawadi maalum, fahamu kua kuna zawadi zimeandaliwa kwa kila kisa miongoni mwa visa vitano vilivyo shinda.