Washindi wa shindano la kisa kifupi kuhusu ushujaa wa wanajeshi na Hashdi Shaábi

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya nne, imetangaza majina ya washindi wa kuandika kisa kifupi kuhusu ushujaa wa wanajeshi na Hashdi Shaábi, kwa kufuata kanuni za uandishi zinazo mvutia msomaji.

Shindano hilo ni sehemu ya ratiba ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya nne, linalo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kuadhimisha mwaka wa nne tangu kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda, litakalo anza Alkhamisi ijayo (23 Shawwal 1440h) sawa na (27 Juni 2019m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Nyie ni fahari na utukufu wetu tunajivunia katika kila umma) litafanyika siku mbili, kamati imesema kua ilipokea idadi kubwa ya visa, vilifika (37) kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala chini ya kanuni za mashindano na masharti yake, na walioibuka washinzi ni:

  • - Khamaailu Yassiri.
  • - Hassan Haadi Atwaar.
  • - Aamali Kaadhim Fatalawi.
  • - Susana Abdullahi.
  • - Suzana Zain.
  • - Afnani Aadil Abbasi.
  • - Fatuma Jaasim Muhammad Farmaan.
  • - Hussein Ali Shami.

Kumbuka kua shindano hili lilikua na masharti yafuatayo:

  • 1- Kisa kufuate kanuni za kiuandishi na maadili ya watoto.
  • 2- Kielezee ujasiri wa eshi la Iraq na Hashdi Shaábi kwa ujumla bila (kumlenga mtu maalum) namna walivyo pambana kulinda taifa na maeneo matakatifu.
  • 3- Kisiwe kimesha wahi kuandikwa au kutolewa siku za nyuma kupitia nyaraka au mitandao ya kielektronik.

Kamati imesema kua visa vitano vilivyo shinda vitachapishwa kwa gharama za Atabatu Abbasiyya na waandishi wa visa hivyo watapewa zawadi maalum, fahamu kua kuna zawadi zimeandaliwa kwa kila kisa miongoni mwa visa vitano vilivyo shinda.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: