Baada ya zaidi ya miaka hamsini (50) tangu kuwekwa marumaru: Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yavishwa vazi jipya la marumaru baada ya kukamilisha uwekwaji wake

Maoni katika picha
Baada ya zaidi ya miezi minne ya kufanya kazi mfululizo, leo haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imevishwa vazi jipya la marumaru, baada ya marumaru za zamani kudumu zaidi ya nusu karne, kwani mara ya mwisho kuwekwa marumaru ilikua miaka ya sabini karne iliyopita, mradi huu umekuja kukamilisha miradi iliyo fanywa katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), iliyo tekelezwa kila mmoja kwa wakati wake, kama mradi wa upanuzi wa haram na upauaji wa uwanja wa haram pamoaja na mradi wa kuweka marumaru katika korido na sardabu za haram na kutengeneza dirisha tukufu na kuliweka, pamoja na mifumo ya viyoyozi (AC), zima moto, tahadhari, mawasiliano na ulinzi, na miradi mingine mingi nafasi haitoshi kuitaja yote.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh “Mradi huu umefanywa na kitengo cha miradi ya kihandisi pamoja na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nao ni mradi unaokamilisha miradi mingine iliyo yanywa katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na umefanywa kutokana na kuharibika kwa marumaru za zamani zilizo kua na zaidi ya miaka (50), ndio ukaingizwa katika orodha ya miradi mingine”.

Akaongeza kua: “Kazi ya kuweka marumaru imefanywa baada ya kugawa uwanja wenye ukubwa wa mita za mraba (5400) sehemu nane, kila sehemu ikiwa na vipande vingi, kila kipande kilikua na hatua mbalimbali za utendaji, ambazo ni:

  • - Kutoa marumaru za zamani.
  • - Kuondoa vipande vya zege ya zamani na kukarabati baadhi ya maeneo.
  • - Kusawazisha sehemu zinye mipasuko kwa kutumia vifaa maalum.
  • - Kuweka zege maalumu isiyo tunza unyevunyevu itakayo beba marumaru.
  • - Kujenga tabaka la chuma chini ya zege.
  • - Kuweka tabaka la chini lenye mfumo wa kusambaza maji, mawasiliano, zimamoto na tahadhari, na kuunganisha na mfumo mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Kuweka marumaru kwa kufuata vipimo maalum”.

Kuhusu wasifu wa marumaru amesema kua: “Marumaru zilizo wekwa ni aina adimu (multi-onyx), zina sifa nyingi, zinarangi nzuri na imara, zinaweza kuvumilia mazingira yote, zinamuonekano mzuri, zina unene wa (sm 4) takriban.

Akamaliza kwa kusema: “Kazi imefanywa kama ilivyo pangwa tena kwa umaridadi na ustadi mkubwa na kuingizwa katika orodha ya miradi iliyofanywa na mikono ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: