Ratiba ya siku ya kwanza itakua kama ifuatavyo:
Sehemu: Ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Atanatu Abbasiyya.
Muda: Saa tatu asubuhi.
- 1- Usomaji wa Quráni.
- 2- Wimbo wa taifa la Iraq, na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Iba).
- 3- Ujumbe kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
- 4- Kaswida kuhusu fatwa tukufu, itakayo somwa na mshairi bwana Ali Swaffaar.
- 5- Ujembe maalum kuhusu mauwaji ya kimbari ya (Spaika) kutoka kwa kamati ya kongamano la Spaika.
- 6- Ujumbe kutoka katika kitabu cha fatwa tukufu ya kujilinda pamoja na kuzindua kitabu hicho.
- 7- Ufunguzi wa maonyesho ya picha yatakayo fanyika katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu.
Itakapo fika saa kumi na moja Alasiri:
Kutakua na warsha ya kielimu kwa anuani ya: (Khutuba za Dini na athari yake katika kupandikiza fikra za kigaidi) ndani ya ukumbi wa jengo la Imamu Haadi (a.s).
Ikifika saa mibi jioni:
Kutakua na kikao cha usomaji wa mashairi ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Na mwisho kutakua na usomaji wa Quráni saa tatu usiku hapohapo ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).