Kumalizika kwa shindano la (mradi wa uhai) utunzi wa kisa kifupi na kutangaza majina ya washindi

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kumaliza mashindano ya (mradi wa uhai) wa kutunga kisa kifupi kwa watoto wa kike peke yao wenye umri kati ya miaka (15-30) lililo tangazwa siku za nyuma.

Shindano hilo lilikua linalenga kubaini uwezo wa mabinti katika kuandika visa, wamejitokeza kwa wingi kushiriki shindano hilo, baada ya kuchuja visa vilivyo wasilishwa katika kamati ya majaji, vilivyo kua vinahusu (familia, watoto, mafanikio ya wanawake, maendeleo ya kielimu, maendeleo kwa ujumla, maisha ya ndoa), ndipo wakatangazwa washindi kumi wafuatao:

  • 1- Narjisi Ibrahim, kisa chake kinasema: (Ili atulize macho yake).
  • 2- Nuru Huda Aali Jabru, kisa chake kinasema: (nimebaki kwenye ahadi).
  • 3- Zaharaa Muhammad Rasuul, kisa chake kinasema: (ujumbe mtukufu).
  • 4- Zaharaa Husaam Shaharabli, kisa chake kinasema: (katika njia ya chuo).
  • 5- Imani Ibrahim Abdu, kisa chake kinasema: (safari ya mwisho).
  • 6- Zhaharaa Haafidh, kisa chake kinasema: (njia yanyu ya kwenda kwenye nuru).
  • 7- Sara Nabiil, kisa chake kinasema: (bado wanaendelea kua na mapenzi).
  • 8- Zaina Abbasi, kisa chake kinasema: (mama yangu kaondoka lakini mwalimu wangu yupo).
  • 9- Zaharaa Swadiq Twalib, kisa chake kinasema: (simulizi ya ndoto baada ya elimu).
  • 10- Zainabu Dhwiyaa, kisa chake kinasema: (mwezi ni shahidi yangu).

Hafla ya kuwapongeza na kuwazawadia washindi hao imefanywa ndani ya jengo la kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s), kila mshindi amepewa zawadi maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: